• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

DC MAKORI AIAGIZA MANISPAA YA UBUNGO KUKAMILISHA MRADI WA JENGO LA UTAWALA

Posted on: December 30th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe Kisare Makori ameiagiza Manispaa ya Ubungo kuongeza kasi ya umaliziaji wa jengo la utawala la Manispaa hiyo ili  kurahisha utoaji huduma kwa wananchi pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa  watumishi wa Manispaa hiyo.

Mhe. Makori ametoa agizo hilo leo tarehe 30 desemba,  2020 wakati alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo  akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo na  kueleza kwamba Serikali ya awamu ya tano inahitaji miradi itekelezwe kwa wakati  na  kwa kuzingatia viwango lengo ikiwa nikurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe. Kisare Makori (mwenye t-shirt ya mistari) akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi  na usalama wa wilaya hiyo pamoja na wataalamu wa Manispaa ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukagua utekelezaji wa jengo la Ofisi za Utawala Manispaa ya Ubungo leo tarehe 30.12.2020

"Baada ya kuvunja mkataba na TBA kutokana na ucheleweshaji wa mradi, Manispaa imewapa  kazi nyinyi local fundi ili mradi uishe kwa wakati lakini utekelezaji wenu bado unasuasua, naagiza kufikia tarehe 7 januari  2021 kila fundi awe amemaliza kazi aliyopewa kwa mujibu wa mkataba wake "alieleza Mhe Makori

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice  Dominic alisema kuwa Manispaa itajitahidi kuwasimamia mafundi  kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia  januari  2021 kazi zote ambazo zinafanywa kwa sasa ziwe zimekamilika na jengo kutumiwa katika hali ya utulivu.

Beatrice ameeleza kuwa kwa sasa kazi zinazofanyika ni uwekaji wa Umeme, mifumo ya maji taka, ufungaji wa milango na upakaji rangi. Kazi zote mafundi wapo wanafanya kazi na fedha zipo " tutajitahidi kuwasimamia wafanye kazi kwa muda tuliokubaliana"

Ili kuhakikisha kazi zote zinafanyika kwa usahihi na ubora unaotakiwa, Beatrice  alieleza kuwa Manispaa  ya Ubungo imetafuta wataalamu mshauri  kwenye masuala ya umeme na uwekaji wa mifumo ya TEHAMA ambaye atashirikiana na mafundi kuhakikisha kazi hizo zinafanyika kwa viwango vinavyotakiwa.

Mradi huo unajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2 ambapo kati  ya fedha hizo  bilioni 1.9 kutoka mapato ya ndani na zaidi  ya bilioni 4 ni fedha kutoka serikali Kuu. 

Jengo la Utawala  la Manispaaya Ubungo likiwa kwenye hatua za umaliziaji. 

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa