Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James Leo tarehe 30.12.2021 ameongea na vyombo vya habari na kutoa mwongozo juu ya wiki ya Usafi ambayo inaanza kuadhimishwa kuanzia kesho 1.12.2021, Maadhimisho hayo yataenda Sambamba na Kauli mbiu ya SAFISHA, PENDEZESHA DAR - ES- SALAAM
Kuelekea katika Maadhimisho hayo ambayo Kimkoa yatafanyika tarehe 4.12.2021 Wananchi wote wa Wilaya ya Ubungo mnaelekezwa kufanya Usafi wa maeneo yenu kwa kuzingatia upandaji wa miti, maua, na kufagia maeneo yote yaliyowazunguka
•Aidha Kheri amesema kuwa Maadhimisho ya wiki ya USAFI yatazinduliwa rasmi Kiwilaya na Wilaya ya Ubungo zoezi hilo litazinduliwa rasmi kesho tarehe 1.12.2021 katika Kata ya Msigani- eneo la Msigani na Kata zingine zote zitakuwa na uzinduzi katika maeneo yaliyopangwa
•Ubungo ni lango kwa jiji la dar es salaam hivyo ameagiza wananchi wote wa Wilaya ya Ubungo kuzingatia mazingira yaliyowazunguka yanakuwa SAFI ili kupendezesha jiji na Maeneo yote kuwa Safi na salama
•Kila mfanyabiashara asafishe eneo linalozunguka biashara yake
•Maeneo yote ambayo wajasiriamali hawajaondoka kwenda kwenye maeneo rasmi waliyopangiwa wanaagizwa kuondoka kwenda sehemu rasmi kwani Utii wa Sheria bila shuruti ni Jambo jema. ameeleza hayo Kheri
•Pia amewaomba Wadau wa Sanaa waendelee kuelimisha Umma kuhusiana na maswala ya USAFI hasa kwa Kutumia ufundi wa kisanaa ili ujumbe uweze kuwafikia wananchi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa