• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

ENG NYAMHANGA APONGEZA UJENZI WA MADARASA 9 KING'ONGO, AAHIDI FEDHA ZA UJENZI WA MADARASA MENGINE 6-8

Posted on: February 12th, 2021

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Tawala  za Mkoa na serikali  za mitaa  Eng Joseph Nyamhanga ameipongeza  Manispaa Ubungo kwa kumaliza  ujenzi wa madarasa 9 katika shule ya msingi King'ongo kwa muda mfupi na kuahidi kuleta fedha za kuongeza madarasa mengine kuanzia  6 hadi 8 kutokana na shule hiyo kuwa na uhitaji mkubwa wa madarasa.


Eng. Nyamhanga ametoa kauli hizo leo februari 12, 2021 wakati alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Manispaa ya Ubungo ikiwemo ujenzi wa madarasa 9 na vyoo matundu 12 katika shule ya msingi king'ongo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Rais  la kutaka wanafunzi wa shule hiyo kutosomea nje na kukaa chini.

"Niwapongeze kwa jitihada zenu za kufanikiwa kujenga na kukamilisha madarasa haya 9 kwa muda wa wiki tatu yaani siku 21 yakiwa na ubora na sasa wanafunzi wanatumia, endeleeni na kasi hii kwenye miradi mingine" alisema Eng Nyamhanga

madarasa mapya katika shule ya msingi King'ongo 

Akiwa kwenye Ziara hiyo Eng. Nyamhanga amesema kuwa "nimeona nipite pia kwenye shule hii nione hali ya  ujenzi, nashukuru madarasa yamekamilika na yanatumika lakini uhitaji wa madarasa  bado ni mkubwa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopo, TAMISEMI tutatoa fedha kuongeza madasara kuanzia sita hadi nane pamoja na matundu 10  ya vyoo"


Eng. Nyamhanga ameendelea kusisitiza kuwa, Serikali inatumia fedha nyingi katika kuboresha sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa  miundombinu ya shule yaani madarasa, madawati na matundu ya vyoo, "nawaagiza walimu mtunze miundombinu  hii ili iweze kudumu lakini pia kuhakikisha fedha ya serikali haipotei bure"

Uboreshaji wa miundombinu unaenda sambamba na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, Eng Nyamhanga amesema  " nimategemeo yangu shule ya msingi king'ongo ufaulu utaongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya kupata mazingira haya mazuri ya kufundisha na kujifunzia"

Baachi ya wanafunzi wa shule ya msingi king'ongo wakiwa kwenye moja ya madarasa  mapya

Shule ya msingi King'ongo ina jumla ya wanafunzi 2520 na inahitaji vyumba vya madarasa 56, vilivyopo 16 na hivyo kufanya upungufu kuwa vyumba cha madarasa 40


Akitoa maelezo ya mkakati wa Manispaa  ya Ubungo  katika kutatua changamoto ya miundombinu ya  madarasa, madawati , viti na ,meza pamoja na  matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari , Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic  amesema Manispaa imeshaainisha shule zenye hali mbaya zaidi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo ili kupunguza uhaba wa miundombinu hiyo hususani madarasa na madawati.

Beatrice amesema kwa sasa manispaa inaendelea na ujenzi wa madarasa  mnne shule ya msingi Tegeta A na  vyumba vitatu shule msingi matosa ambayo ni mpya na miradi yote iko hatua ya umaliziaji.

 baadhi ya walimu wa shule ya msingi King'ongo  wakimusikiliza katibu Mkuu alipotembelea shule hiyo leo februari 12,2021


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa