- Mapema leo 24 Novemba, 2022 Wafanyakazi wa benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wamefika ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa Ubungo kwaajili ya kutoa msaada wa Komputa
- Kila mwaka wafanyakazi wa NMB kanda ya Dar es Salaam huwa na desturi ya kuchanga fedha na kujitoa kwa jamii kwa njia mbalimbali na kwa Mwaka huu wa 2022 walifanikiwa kuchanga fedha na kwa Manispaa ya Ubungo wamefanya yafuatayo;
1. Kulipia Bima ya Afya kwa watoto yatima 100 katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo wilaya ya Ubungo.
2. Kununua Komputa mbili na kuzikabidhi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ili kuongeza ufanisi wa kuhudumia wananchi
- Mkurugenzi wa Ubungo Ndugu Beatrice Dominic ameishukuru sana benki ya NMB kwa kujitoa kwao kwa Manispaa ya Ubungo na amewakaribisha tena wakati mwingine
@nmbtanzania
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa