- Mwanzo
- Kuhusu sisi
-
Utawala
- Muundo
-
Idara
- Elimu Sekondari
- Agriculture, Livestock and Fisheries
- Industry,Trade and Investments
- Planning and Coordination
- Infrastructure, Rural and Urban Development
- Pre-Primary and Primary Education
- Human Resources Management and administration
- Health, Social Welfare and Nutrition Services
- Communit Development
- Vitengo
- Sheria ndogo ndogo za Manispaa
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mada hizo zilitolewa na watu mbalimbali akiwemo Prof. Kitila Mkumbo mbunge wa jimbo la ubungo, Dr. Victoria Lihiru na Dr. Richard Mbunda ambao ni wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao wameeleza kwa kipindi cha miaka 61 ya uhuru Tanzania imeweza kufikia maendeleo kwa nyanja mbalimbali ikiwemo elimu bure kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita, mpango wa kuhakikisha kila mwananchi anapata uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima, ukopeshaji wa mikopo isiyo na riba kutokana na fedha za asilimia kumi za mapato ya ndani, kuwepo kwa viongozi wanawake kwenye nafasi za juu za uongozi nchini, na mengine mengi mazuri yanayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita.
Akiongea wakati akifungua kongamano hilo Mhe. Kheri James Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ameeleza tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa mwaka huu maazimisho hayo yatafanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, kufanya mdahalo na michezo mbalimbali kama ambavyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya sita alivyoeleza na kumpongeza kwa uamuzi wa kupeleka fedha za maadhimisho hayo kufanya ujenzi wa mabweni ya wasichana kwa shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Kuazimisha maazimisho hayo kwa njia ya mdahalo ni kupata nafasi ya kutoa elimu zaidi ya kurithisha ujuzi, historia na maarifa ya tulipotoka, tulipo na tunapokwenda kwa kizazi na kwa makundi ya kijamii ili kila mmoja ayajue vizuri.

