Mapema leo Machi 28, 2023 ofisi ya kamishna msaidizi wa ardhi imefanya kikao na baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwasilisha wasilisho la Mpango Kabambe (Master Plan) wa mkoa wa Dar es Salaam kwa sehemu ya Manispaa ya Ubungo
Wasilisho hilo limetolewa leo katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo na Afisa mipango miji mkuu kutoka ofisi ya Kamishina msaidizi mkoa wa Dar es Salaam ndugu Michael Mwalukasa
Mwalukasa ameeleza kuwa mpango huo Kabambe wa Mkoa wa Dar es Salaam unatoa mwongozo wa ukuaji, upanukaji na uendelezaji wa kila kipande cha Ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam pamoja na kudhibiti uendelezaji holela wa maeneo.
Akichangia katika mjadala huo naibu meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Omary Yenga ameipongeza ofisi ya kamishna msaidizi kwa kufanya kikao hicho na baraza la madiwani lakini pia ameshauri kuwe na mpango wa utekelezaji ili kuisaidia Manispaa kutekeleza mpango huo kwa wakati
Aidha wizara inatoa rai kwa Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaandaa mpangokina na kutoa vibali vya ujenzi kulingana na mpango huu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa