• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MANISPAA YA UBUNGO YAZINDUA MIONGOZO MITATU YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA ELIMU

Posted on: September 29th, 2022



Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imezindua muongozo  mitatu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Elimu ambayo utasaidia kuleta mageuzi chanya katika usimamizi wa elimu na kuongeza tija katika ufundishaji mashuleni

Uzinduzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutaka Miongozo hiyo izinduliwe ngazi ya Wilaya pamoja na kuizindua ngazi ya Taifa ili kuleta uelewa na ufanisi katika utekelezaji wa miongozo hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewapongeza Walimu wa Manispaa hiyo kwa utumishi bora kwenye kazi zao za kila siku za kuwafundisha wanafunzi pamoja na kuwalea wanafunzi katika maadili bora ya kitanzania.

"Mwalimu ni mtu pekee anayekutana na watoto wa aina zote kila siku hivyo ana nafasi kubwa ya kuwajenga katika misingi iliyo bora kitaaluma na kijamii kwani pamoja kuwapa elimu lakini pia ni mlezi" alieleza Mhe. James

Aidha, amewataka walimu kubuni mbinu nzuri zitakazosaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kwa kushirikiana na wazazi na walezi ili kuwa na makubaliano ya pamoja na kuepusha malalamiko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo  Beatrice Dominic amesema kuwa kupitia miongozo hiyo ambayo imezinduliwa leo itaenda kuleta tija kubwa kwenye sekta ya elimu na itawafanya walimu wajisikie fahari kufanya kazi yao

Pia, Beatrice  amesema kuwa Manispaa ya Ubungo imeshapokea fedha jumla ya shilingi Bilioni 1.6 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 81 ikiwa ni  maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023

Ametumia nafasi hiyo kuwasihi walimu watakaopata fedha za ujenzi wa madarasa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na ubora ili watoto wote watakaofaulu kujiunga kidato cha kwanza  kuanza masomo kwa wakati na kwenye mazingira bora.

Miongozo hiyo iliyozinduliwa  na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mkoani Tabora  ni pamoja na mwongozo wa uteuzi wa viongozi wa elimu, mwongozo wa mkakati wa ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu msingi na mwongozo wa changamoto katika uboreshaji wa elimu msingi na sekondari

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa