Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka wafanyabiashara wote wanaopanga biashara zao nje ya soko la Mabibo kurudi ndani ya soko hilo ili kuimarisha huduma za uuzaji na ununuzi ndani ya soko hilo.
Agizo hilo amelitoa Leo Juni 10, 2022 alipotembelea soko la Mabibo na Simu 2000 yaliyopo Wilaya ya Ubungo, lengo ikiwa ni kukagua masoko hayo pamoja na kusikiliza kero za wafanyabiashara ambapo moja ya kero iliyoibuliwa na wafanyabiashara wa soko la mabibo ni uwepo wa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo.
“Kero kubwa ya soko hili ni uwepo wa wafanyabiashara zinazofanana na sisi nje ya soko hali inayosababisha wafanyabiashara wa ndani kutokuuza kwani wateja wananunua bidhaa nje” Alisema Amina Elias mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo.
Akijibu hoja hiyo Makalla ameeleza kuwa moja ya sababu zinazopelekea masoko mengi kufa ni uwepo wa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko ambazo zinazofanana na zilizopo ndani ya soko hivyo rudini wote ndani ya soko.
Wakati huo huo Makalla amewaagiza watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha ndani ya siku saba hakuna mfanyabiashara yeyote nje ya soko hilo.
Kwa upande wa soko la Simu 2000 Makalla ameelekeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kuwa, maombi ya wafanyabiashara kufanyiwa kazi ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya maji, barabara, mitaro na kuongezewa ruti za magari ya abiria ili kuongeza wateja.
Aidha, Makalla amewataka wafanyabiashara wote kufanya biashara kwa utulivu na Serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano katika kuimarisha na kuboresha mazingira yakufanya biashara kwani uchumi wa Dar es Salaam unategemea biashara.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa