• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MIAKA MINNE YA MAFANIKIO: UTELEKELEZA WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

Posted on: September 2nd, 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,chini ya serikali ya awamu ya Sita imefanikiwa kuleta na kutekeleza miradi yenye tija kwa wananchi. Katika kutekeleza miradi ya maendeleo kuanzia Julai, 2020 hadi Juni 2024, Manispaa ya Ubungo imepokea kiasi cha jumla ya Shilingi 104,592,517,440.76 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. Fedha hizi zinajumuisha kiasi cha Shilingi 66,429,171,245 ambazo ni fedha za Serikali Kuu na Shilingi 38,163,346,195.30 kutoka kwenye Mapato yetu ya ndani.

Kwa namna ya kipekee kabisa tunaishukuru Serikali yetu ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupatia fedha hizi ili kuweza kutekeleza miradi na uendeshaji wa manispaa katika kuhudumia wananchi.

Tunashukuru pia viongozi ndani ya Mkoa kwa maelekezo na ushauri wanaotoa wakati wa utekeleza wa shughuli za serikali katika Manispaa. Vilevile, tunashukuru wananchi na Wadau wa maendeleo kwa kushiriki katika kuibua, kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali. Haya ndiyo matokeo ya chanya ya sera na maelekezo ya serikali na Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma kwa wananchi zinaimarika.

Tunatoa shukrani kwa Waandishi wa Habari kwa kutoa taarifa kwa jamii kuhusu hali ya utekelezaji wa shughuli za serikali katika manispaa ya Ubungo. Naomba nitumie muda huu pia kuwahakikishia kuwa dhamana tuliyopewa tunaitekeleza kwa tija kubwa ili kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwatumikia wananchi. 

Dkt Aron T. Kagurumjuli

Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo



 

SEKTA YA AFYA

                                                                                                                                                         Hospitali ya Wilaya ya Ubungo (UDH)

Manispaa ya Ubungo imeendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na Afya bora. Kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Juni 2024 kiasi cha Shilingi 11,803,548,336.81 zimepokelewa. Kati ya fedha hizi, Fedha za Serikali kuu ni Shilingi 8,891,098,733.10 na Fedha za Mapato ya ndani ni Shilingi 2,912,449,603.71

 

Fedha hizi zimetekeleza Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Ujenzi wa wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji  kituo cha afya Makurumla , Ununuzi wa vifaa tiba, madawa na vitendanishi, Ujenzi wa vituo vitatu  vya  afya  vya Amani, Goba na Makaburi, Upanuzi wa Zahanati ya Mpiji Magohe kuwa kituo cha Afya, Ujenzi wa wodi tatu za wazazi katika zahanati ya Msewe, Mabibo na Goba, Ujenzi wa Zahanati tatu za  Msingwa, Temboni, na Kinzudi, Ujenzi wa jengo la ghorofa 1 katika Kituo cha Afya Sinza, Ujenzi wa jengo la ghorofa 2 katika Kituo cha Afya  Kimara.

 

Utekelezaji wa miradi hii ya afya imesaidia kupunguza umbali wa kufuata huduma za afya, imepunguza vifo vya mama na watoto na imepunguza msongamano katika vituo vya afya vilivyokuwepo awali.

                     

SEKTA YA ELIMU (MSINGI)


Kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Juni, 2025 katika elimu msingi Manispaa ya Ubungo imetoa kiasi cha shilingi 10,895,981,325.09. Mapato ya ndani shilingi 6,646,517,453.00, Ruzuku ni shilingi 4,249,463,872.09

Baadhi ya miradi mikubwa iliyotekelezwa katika manispaa  kupitia fedha hizo ni pamoja na Ujenzi wa Shule tano mpya za Msingi, madarasa 302, matundu ya vyoo 192, nyumba 4 za walimu, uzio katika shule 4 za msingi,  makontena 18 kuwa maktaba katika Shule za Msingi, pia Fedha hizo zimesaidia kwenye Ukarabati wa madarasa 104, Ununuzi wa madawati 6285 kwa shule za msingi, na Fedha za Elimu bila malipo zimetolewa kwa shule zote 66. Aidha,Wanafunzi wa darasa la kwanza wameongezeka kutoka 18,995 mpaka 21,210.


 

Kwa upande wa Sekondari, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Divisheni ya Elimu Sekondari kwa mwaka 2021/2022-2023/2024 tumepokea fedha jumla ya shilingi 19,803,575,881.14. Fedha za mapato ya ndani Tsh. 3,661,165,548.66 na Ruzuku Shilingi   16,142,410,332.48 

Fedha hizo zimetumika katika Ujenzi wa shule maalum ya wasichana ya mkoa ya Sayansi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1080 (kidato cha I - VI) na Tayari shule hii imepokea wanafunzi wa kidato cha tano 2023. Hata hivyo, fedha hizi zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita zimesaidia Ujenzi wa shule mpya za kata na kufanya idadi ya shule za sekondari kufikia 34 mwaka 2024 kutoka 27 mwaka 2020.Pia tumejenga, vyumba vya madarasa -267, nyumba za walimu -09, Mabweni-09, matundu ya vyoo -183, Majengo ya utawala -04, vyumba vya madarasa -21, na Ununuzi wa viti na meza 14,075.

Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu sekondari imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi, Kupunguza umbali mrefu wa kutembea mfano, shule mpya ya sekondari Ukombozi wanafunzi walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Km 10 kufuata shule.


UTAWALA

Jumla ya Idadi ya Watumishi 2,392 wamepandishwa madaraja ndani ya kipindi cha awamu ya sita huku watumishi 1761 wakilipwa malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya Shilingi 2,782,031,932.00

 

UDIBITI WA TAKA NGUMU

Kwenye eneo la hifadhi ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu, Ndani ya awamu ya sita, Halmashauri imetoa shilingi 4,998,871,131.61 (Mapato ya ndani) kwa kipindi cha miaka mitatu na kutekeleza shughuli nyingi ikiwemo Ununuzi wa magari mawili (2) ya kubeba taka. Manispaa inasafisha mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu 150 km kwa mwaka.

UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI 

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekuwa ikiwawezesha wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Serikali ya awamu ya sita, imewasikia na imewafikia wananchi. Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Juni 2025, tumekopesha jumla ya kiasi cha Shilingi 8,457,062,440.00 kwa vikundi 1,402 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kati ya fedha hizo shilingi 4,267,835,655.00 zimetolewa kwa wanawake, shilingi  3,639,926,785.00 zimetolewa kwa vijana na  shilingi  549,300,000.00 zimetolewa kwa watu wenye ulemavu.  Fedha zote ni mchango wa asilimia 10 ya Mapato ya ndani.

Katika kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini, Mpaka sasa halmashauri ya Ubungo ina jumla ya kaya za walengwa 2,838 zinazoendelea kupokea ruzuku. Shilingi 1,991,729,037.00 zimepokelewa kwa jumla ya kaya za walengwa 2,838. Fedha hizi zimejumuisha shilingi 1,798,472,837.00 kwa ajili ya wanufaika na shilingi 193,256,200 kwa ajili ya ufuatiliaji.


 

 

 

SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

Kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Manispaa ya Ubungo tumepokea kiasi cha Shilingi 428,877,625.00. Fedha hizi zinajumuisha Mapato ya ndani shilingi 389,208,500.00 na Ruzuku Shilingi 39,669,125.00 

Kupitia fedha hizo, tumekarabati machinjio ya kuku Manzese kwa kuwekewa miundombinu ya maji na umeme, Ujenzi wa Miundombinu katika eneo la Nane nane Tungi – Morogoro. Lakini pia Halmashauri imewezeshwa kumiliki eneo la ekari 28 kwa ajili ya shamba darasa eneo la Kibesa - Mpiji Magohe na Ujenzi wa kisima eneo la Kibesa - Mpiji Magohe.


BIASHARA NA UWEKEZAJI

Biashara na Uwekezaji halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 3,071,161,080.64 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo uendelezaji wa kituo cha mabasi Mgufuli, Fremu za Maduka Manzese, na Uboreshaji wa Masoko.

 

 

MIPANGO MIJI

Kuanzia Julai 2020 hadi Juni 2024 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi1,306,796,296.20 kwaajili ya urasimishaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi.

SEKTA YA FEDHA


 

SEKTA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

 



Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MIAKA MINNE YA MAFANIKIO: UTELEKELEZA WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    September 02, 2025
  • MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA MAFANIKIO YA WAJASIRIAMALI

    September 30, 2025
  • UBUNGO YAAHIDI KUJIPANGA IMARA ZAIDI KWA MSIMU UJAO WA SHIMISEMITA | YAPOTEZA MBELE YA DODOMA JIJI

    August 29, 2025
  • WANANCHI MSIGANI WAANZA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO MJINI.

    August 29, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa