• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MIKOPO ISIYO NA RIBA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.2 YANUFAISHA WAJASIRIAMALI WADOGO UBUNGO

Posted on: November 5th, 2020

Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam, imefanikiwa kuviwezesha vikundi vya wajasiriamali wadogo 222 kukuza uchumi kwa kutoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi 1,274,420,000/= kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa serikali wa kukuza uchumi kwa wananchi wake kupitia fedha za mapato ya ndani (10%)

Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Maendeleo ya jamii wa Manispaa hiyo, Rose Mpeleta baada ya kutembelea baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wadogo vilivyopewa mkopo na manispaa hiyo, na kueleza kwamba, Manispaa ina jumla ya vikundi 5418 vilivyosajiliwa lakini vikundi 222 ndivyo vilivyofanikiwa kupata mkopo.

Mpeleta ameseama kuwa vikundi vilivyopata mikopo vimefanikiwa kuboresha biashara zao  kwa kuongeza mitaji  pamoja na kuboresha Maisha yao na kuondokana na umasikini  “hilo ndio lengo kuu la serikali kuhakikisha wananchi wanafikia uchumi wa kati kwa kujishughulisha na kazi za ujasiliamali ili kukuza kipato” .


Vikundi vina miradi mizuri ambayo inawaingizia kipato ikiwemo ufugaji, biashara za maduka, mama lishe, ujenzi, na mingine mingi na urejeshaji wake unakwenda vizuri kwani biashara zao zinaendelea vizuri.

Kikundi cha walemavu kilichopo  kata ya kimara wakijadiliana kuhusu maendeleo ya kikundi. Kikundi kimepata mkopo wa shilingi milioni 5

Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha HONDOHONDO MLEZI WA WANA kilichopo kata ya Kimara Manispaa ya Ubungo Sara Godwin ameleza kuwa kabla ya mkopo alikuwa na biashra ya genge dogo tu lakini baada ya kupata mkopo biashara yake imepanuka ambapo ameweza kuongeza duka pamoja na kuongeza bidhaa kwenye genge lake.


Mwenyekiti ameeleza kuwa  “naishukuru Manispaa ya Ubungo  na Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwani imetuongezea mitaji ya biashara zetu lakini pia Maisha yetu yamebadilika kwani tunauwezo wa kupata mahitaji ya msingi na kuweka akiba.

Aidha Sara ameiomba serikali kuongeza viwango vya mikopo hiyo ili wajasiliamali wakuze biashara zao na kwa kufanya hivyo tutakuwa kwenye maisha ya uchumi wa kati kwa vitendo.


Mathew Samson Swai ni moja ya wanakikundi cha vijana cha wajasiriamali cha Baruti Umoja Group, amewashauri vijana kujiunga kwenye vikundi kwani ni njia rahisi ya kufikia maendeleo, aidha Swai amewashauri vijana kuwa wavumilivu  kwa wateja, kutokata tamaa pamoja na kujifanyia tathimini ya biashaya yake ili kujua kama biashara inakua au inashuka.

Kikundi cha Baruti umoja Group chenye wanachama 22, pamoja na kuwa na  biashara ya mwanakikundi mmojammoja lakini pia kimefanikiwa kununua Bajaji 4 kutokana na mikopo ya ujasiriamali inayotolewa  na manispaa ya Ubungo ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 walipata mkopo wa shilingi milioni 25,500,000/= na wameanza kufanya marejesho.


Mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo haina riba, vikundi vinarudisha kiasi kilekile cha fedha walichokopa, na urejeshwaji wake unafanyika baada ya miezi mitatu baada ya kupata mkopo.



Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa