• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

SOKO LA KUKU MANZESE LABORESHWA

Posted on: October 10th, 2023

Manispaa ya Ubungo imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 1.3 kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uboreshaji wa soko la Manzese maarufu soko la kuku.


Katika uboreshaji huo Manispaa ya Ubungo imepanga kujenga fremu za kisasa kwenye ghorofa ya sakafu tatu ambapo jumla ya fremu 39 zitajengwa na hadi sasa ujenzi upo asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2024.


Akielezea ujenzi huo Ndg. Geofrey Mbwama Afisa Mfawidhi sehemu ya biashara na masoko wa Manispaa hiyo amesema Manispaa imedhamiria kujenga fremu za kisasa kwa wafanyabiashara wa soko hilo hususani wauza kuku ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwenye maeneo rafiki yatakayovutia wateja wao na hivyo kuweza kukuza vipato vyao.


Mbwama ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kuanza kufanya biashara zao kisasa hususani wafanyabiashara wa kuku ambapo miundombinu itakayokuwepo itawalazimu kutunza kuku kwenye majokofu mara baada ya kuchinja.

Aidha, Mbwama ameeleza kuwa uboreshaji wa soko unaenda sambamba na sheria ya upangaji miji kwa kuweka miundombinu ya kisasa ukizingatia Manzese ni “smart area” na pia ni katikati ya Mji.


Sambamba na hayo Mbwama ameeleza kuwa uboreshaji wa soko hilo pia ni moja ya mkakati wa Manispaa wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ili kuiwezesha Manispaa hiyo kukusanya Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya sekta za elimu, afya, uboreshaji wa masoko na miundombinu mbalimbali.


Kwa upande wake Mualami Muya mfanyabiashara wa soko hilo akimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Manispaa ya Ubungo kwa ujumla amesema uboreshaji wa soko hilo utasaidia wafanyabiashara wa soko hilo  hususani wauza kuku kuwa na eneo salama la kufanya biashara zao tofauti na ilivyokuwa hapo awali.


“Tunamshukuru sana Rais wetu na viongozi wetu wa Manispaa ya Ubungo kwa uboreshaji wa soko hilo na tunaahidi kuitunza miundombinu yake sambamba na utoaji wa ushuru wa soko kwa maslahi ya Manispaa yetu” alisema Mualami.


Mualami ameeleza kuwa ujenzi wa fremu zenye miundombinu ya kisasa kwa ajili ya biashara ya kuku sio tu utaboresha mazingira ya biashara lakini pia utaondoa hasara kwa wafanyabiashara pale ambapo kuku watahitajika kuhifadhiwa kwenye majokofu kwani hali ya sasa inawalazima kulipia kiasi cha Fedha ili kuhifadhi kuku wao na wakati mwengine kuku hao upotea


“Kuna muda mfanyabiashara anapata kuku kutoka Mikoani hadi wakifika mjini kuku hao wanachoka sana na ndipo itamlazimu muuzaji kuchinja kuku hao na kuwahifadhi kwenye majokofu ambayo kwa sasa tunalipia na bado mara zingine muuzaji anaweza kupoteza kuku hao kwenye majokofu hayo kiukweli tunafarijika sana na uboreshaji huu ambao utapunguza au kuondoa tatizo hili” Alisema Mualami.

Soko la Manzese Lina jumla ya wafanyabiashara 496 ambapo kati ya hao wafanyabiashara wanaouza kuku ni zaidi ya 100 huku wanaobaki wanajishughulisha na biashara za mama lishe na biashara mchanganyiko.


Pia soko la Manzese ni miungoni mwa masoko 13 ya Manispaa ya Ubungo ambalo pia ni miongoni mwa masoko manne yanayoboreshwa na Manispaa hiyo kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 likiwemo soko la Mabibo, soko la SIMU 2000 na soko la Mbezi.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa