• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

SOKO LA SIMU 2000 LA HAMASISHA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO.

Posted on: October 10th, 2023

“Naipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitahadi zinazofanyika za uboreshaji wa masoko ikiwemo soko la SIMU 2000 kitendo ambacho kinapelekea wafanyabiashara waliotelekeza vibanda vyao ndani ya soko hilo na kwenda kupanga kwenye maeneo yasiyorasmi kuanza kurudi sokoni”


Kauli hiyo ilitolewa na Ndg. Charles Goodluck mfanyabiashara wa soko hilo wakati alipotembelewa na waandishi wa habari kwa ajili ya kupata maoni ya wafanyabiashara baada ya maboresho yanayoendelea kwenye soko hilo.


Hapo awali soko hilo halikuwa na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hususani kipindi cha mvua lakini vibanda vya awali havikuwa rafiki kwao, kitendo kilichopelekea wafanyabiashara wengi kuondoka kwenye soko hilo na kwenda kufanya biashara kwenye maeneo yasiyorasmi ikiwemo maeneo ya barabarani.

Charles ameendelea kuipongeza Manispaa ya Ubungo kwa ushirikishwaji wa wafanyabiashara juu ya namna bora ya kuboresha soko hilo kwa kuzingatia mahitaji yao ambapo vibanda vilivyojengwa vinamuwezesha mteja kufika kwenye kila kibanda kutokana na jinsi vilivyojengwa kitendo ambacho kinapelekea mzunguko wa biashara kuwa mzuri.


Nae Ndg. Zainab Hassan mfanyabiashara wa soko hilo alisema uboreshaji wa soko hilo pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara lakini pia utaiwezesha Manispaa kuongeza mapato yake kwani sasa kila siku tunashuhudia ongezeko la wafanyabiashara wakihitaji kupata vibanda vya kufanya biashara zao.


“Sisi kama wafanyabiashara kwa maboresho haya tupo radhi tena kwa hiari kulipa ushuru na kodi mbalimbali za Manispaa kwani tunaona matunda yake” alisema Zainab.


Kwa upande wake Ndg. Geofrey Mbwama Afisa Mfawidhi sehemu ya Biashara na Masoko Manispaa ya Ubungo amesema katika kutekeleza sera na maagizo ya Mhe. Rais wa awamu ya sita ya kuhakikisha masoko yanaboreshwa, Manispaa ya Ubungo inatekeleza kwa vitendo kwa kufanya uboreshaji wa masoko kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani na Serikali kuu.


Geofrey ameendelea kueleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Ubungo imeweza kutenga zaidi ya Bilioni 2 Fedha za mapato yake ya ndani kwa ajili ya uboreshaji wa masoko ikiwemo soko la Mabibo, soko la SIMU 2000, soko la Manzese na soko la Mbezi Shule kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.


Akielezea ujenzi wa vibanda vya Soko la SIMU 2000 Geofrey ameeleza kuwa Manispaa ya Ubungo kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani kwa awamu ya kwanza ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya uboreshaji wa vibanda vya soko hilo na jumla ya vibanda 170 vimejengwa na kwa awamu ya pili kiasi cha shilingi milioni 39 kilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa vibanda 80 vya wafanyabiashara ambapo ujenzi upo asilimia 30 na utakamilika mwishoni mwa mwezi huu.


Akiongelea lengo la maboresho ya soko hilo Geofrey ameeleza kuboreshwa kwa soko hilo ni kuwezesha wafanyabiashara ndogondogo kuinua vipato vyao sambamba na kuongezeka kwa mzunguko wa biashara, kuwaweka wafanyabiashara pamoja kutokana na aina ya biashara zao na kuongeza mapato ya Manispaa kutokana na ushuru utakaotozwa kwenye vibanda hivyo.


Soko la SIMU - 2000 ni miongoni mwa masoko 13 yanayomilikiwa na Manispaa ya Ubungo ambalo lilianzishwa mwaka 2014 likiwa limejengwa vibanda 312 na baadae wafanyabiashara walihamishwa kutoka kwenye maeneo mbalimbali waliyokuwa wakifanyia biashara ambayo hayakuwa rasmi na kuhamishiwa sokoni hapo lakini walitelekeza vibanda vyao kutokana na hali iliyokuwa hapo awali.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa