• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

UBUNGO YAADHIMISHA SIKU YA UONI DUNIANI KWA UPIMAJI BURE WA MACHO ZAHANATI YA GOBA

Posted on: October 15th, 2025

Wakazi wa Ubungo wahimizwa kupima macho mara kwa mara kuepuka uoni hafifu

Na Twagile SangaGoba, Ubungo – Oktoba 15, 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeadhimisha Siku ya Uoni Duniani kwa kutoa huduma ya Upimaji wa macho bure kwa wananchi, tukio lililofanyika leo katika Zahanati ya Goba.

Akifungua rasmi maadhimisho hayo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo, Dkt. Aristides Raphael amewataka wananchi kujenga utaratibu wa kufanya uchunguzi wa macho angalau mara moja kwa mwaka, ili kuepuka changamoto ya uoni hafifu au upotevu wa kuona unaozuilika.

“Magonjwa mengi ya macho hayaonyeshi dalili mapema. Kupima mara kwa mara huongeza uwezekano wa kugundua matatizo kabla hayajawa makubwa,” alieleza Dkt. Raphael.

Aidha, alisisitiza pia umuhimu wa wananchi kupima afya zao dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu, ambayo mara nyingi huathiri macho kwa njia zisizoonekana mapema.

Katika kuonyesha mshikamano wa kijamii, Dkt. Raphael amewashukuru wadau mbalimbali wa afya waliosaidia kufanikisha siku hiyo akiwataja kuwa ni: Vision Care Foundation, Eye Care International Hospital, Dr Agarwals Eye Hospital, Ona Eyes Care, CBM na Your Eyes.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Macho wa Manispaa ya Ubungo, Bi. Joyce Riwa,  alieleza kuwa duniani kote, takribani watu bilioni 2.2 wanakabiliwa na matatizo ya uoni hafifu, na zaidi ya nusu yao wako barani Afrika.

“Kwa takwimu hizi, kupima macho ni jambo la lazima kwa kila mtu. Inashauriwa kupima angalau mara moja kwa mwaka ili kujikinga mapema,” alisema Bi. Riwa.

Hata hivyo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao kufanya uchunguzi wa macho kwani mtoto akipata tatizo la uoni linaweza kuathiri ujifunzaji shuleni na kushindwa kufurahia maisha ya kila siku na kumuweka katika matatizo ya afya ya macho siku za usoni.

Mmoja wa wananchi waliopata huduma hiyo, Ndugu Mwasiki Kahamara, ameishukuru Manispaa ya ubungo kwa kuratibu zoezi hilo la bure akisema limewafikia hata wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha kupata huduma hiyo muhimu.


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UBUNGO YAADHIMISHA SIKU YA UONI DUNIANI KWA UPIMAJI BURE WA MACHO ZAHANATI YA GOBA

    October 15, 2025
  • DC MSANDO ATEMBELEA MRADI WA MAJI KING'ONG'O, AONGEZA MUDA KWA DAWASA KUKAMILISHA KWA UBORA

    October 13, 2025
  • DC MSANDO AWATAKA WENYEVITI KUWASILISHA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI

    October 04, 2025
  • SERIKALI KUJA NA MPANGO WA DHARURA NA HARAKA KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI WA MWENDOKASI

    October 01, 2025
  • Tazama zote

Video

UBUNGO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA | WANAFUNZI WAASWA KUJITUNZA
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa