Mapema leo Februari 22, 2023 walimu wa Afya mashuleni wamepewa elimu kuhusu uzingatiaji wa ulaji wa lishe bora mashuleni ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na afya bora ili kuepukana na magonjwa
Katika kuhakikisha wanafunzi wanapewa lishe iliyo bora walimu hao wamesisitizwa kuwafundisha namna ya ulaji wa makundi mbalimbali ya mchanganyiko wa vyakula vyenye kujenga na kulinda mwili
Akitoa elimu hiyo Afisa lishe wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ndugu Herieth Mbukuzi aliendelea kusisitiza katika uzingatiaji wa vyakula ambavyo vinakua na mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya lishe yanayolenga kuimarisha mwili
Tuepukane na utumiaji wa mafuta mengi, sukari kwa wingi na chumvi. Alisisitiza
Ulaji wa vyakula bila ya kuzingatia lishe bora kunaweza kusababisha magonjwa, tuzingatie hili
Walimu wakijengewa uwezo katika maswala ya lishe mashuleni
Aidha Shubira Bachuba mratibu wa afya mashuleni amesisitiza swala la ukatili wa watoto mashuleni lizingatiwe kwa kukemea vitendo viovu kwa wanafunzi sambamba kwa kuwapa elimu ya kuepukana na vishawishi
Aliendelea kwa kusema kuwa watoto mashuleni wanatakiwa kupewa uangalizi mkubwa hasa kwa wale wanaojiingiza katika makundi mabovu kuhakikisha tunawaelimisha ili waweze kuachana na mambo hayo
Akitoa shukrani kwa niaba mwalimu Anna amesema kuwa elimu waliyopata ni mtambuka na watahakikisha swala la lishe mashuleni linaenda kuwekewa kipaumbele
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa