• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA KWA UFANISI KUZALISHA WASOMI BORA

Posted on: February 16th, 2021

Mkurugenzi wa Elimu  Ofisi ya Rais TAMISEMI , Julius Nestory amewaagiza watendaji wa sekta ya elimu Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam  kuhakikisha wanawasimia   walimu wa shule za msingi na sekondari kufundisha wanafunzi kwa ufanisi   ili kuzalisha wasomi wenye ueledi wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na  wanaoweza kushindana  na mataifa mengine kitaaluma.


 Agizo hilo amelitoa leo tarehe 16 februari,  2021 kwenye kikao kilichojumuisha viongozi watendaji wa elimu za msingi na sekondari , waratibu elimu kata, walimu wakuu, na wakuu wa shule wa Manispaa hiyo lengo likiwa kukumbushana wajibu wao katika kutoa elimu bora kwa watoto ambao ni Taifa la kesho.

Wataalamu wa elimu manispaa Ubungo wakiwa kwenye kikao cha kupokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa elimu OR_TAMISEMI 


Nestory ameeleza kuwa malengo mahususi ya kikao hicho ni kuwakumbusha walimu kuwa elimu wanayotoa darasani  ilenge  kuwaongezea maarifa   yatakayodumu kwa muda mrefu  lakini pia yawasaidie kutatua changamoto zake za kimaisha.

Akiainisha hatua tano mhimu za kuzingatia katika ufundishaji bora, Nestory amesema kuwa mwalimu lazima awe na muhtasari wa somo,nukuu ya somo, andalio la somo pamoja na kufanya tathimini  ya mada husika ili kujua uelewa wa wanafunzi kwenye somo husika.

"Waratibu elimu kata, Wakuu wa shule na Walimu wakuu simamie  maandalio ya masomo kwa walimu wenu kwani hatua moja ikirukwa  ufundishaji wa ufanisi hautakuwepo na hivyo kuzalisha wanafunzi wenye uelewa mdogo na wasioweza kushindana katika soko la kimataifa" alisisitiza Nestory

Tatizo kubwa lipo kwenye ukaziaji hafifu wa maarifa ,walimu fundisheni kwa makini na mawanda mapana na kuchagua vitu mhimu   na kuwajengea uelewa zaidi ili viwasaidia kujibu  vyema mitihani yao na hatimaye kuongeza ufaulu.

Nestory ameeleza kuwa kwa elimu ya msingi walimu wahakikishe wanatumia mbinu bora ikiwemo kuwa na madarasa yanayoongea  zitakazomwezesha  watoto kujua kusoma, kuandika na kuhesabu  vizuri kabla ya kufika darasa la nne.

Aidha kwa upande wa sekondari, Nestory amesisitiza walimu kutumia lugha ya kiingereza wakati wa kufundisha ili kuwasaidia watoto kujifunza lugha hiyo ambayo ndio wanayotumia kufanya mitihani yao " wanafunzi wengi wanafeli mitihani kwa kushindwa kujieleza kwa ufasaha wajengeeni uwezo kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha wanaongea lugha hilo muda wote wakiwa shule"

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar Es salaam  ndugu  Abdul Maulid amewasisitiza walimu wa sekondari kufuata miongozo ya ufundishaji ikiwemo kutumia lugha ya kiingereza kufundishia pamoja na kutumia wiki nane za mwanzo kunajengwa uwezo wanafunzi wa kidato cha kwanza ili kuwajenga kisaikologia juu ya matumizi ya lugha hiyo ambayo ni tofauti na shule ya msingi walikotoka.

Wakitoa kauli kwa nyakati tofauti walimu Wakuu na wakuu wa shule wameahidi kutekeleza maagizo hayo kikamilifu ambayo yanalenga kuboresha elimu  kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu.




Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa