Wananchi wa Ubungo wanatarajia kuanza kupata usaidizi wa kisheria kwenye changamoto mbalimbali zinazowakabili kutoka kwa wanasheria wa kampuni ya NMG Artoney pamoja na wanafunzi wa sheria ambapo huduma hiyo itatolewa katika kata zote 14 za wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James leo Juni 11 2022 alipozindua programu maalumu ya usaidizi wa masuala ya kisheria kwa wananchi wa wilaya hiyo ambapo wananchi watapata fursa ya kukutana na mawakili na keleza na kusaidia masuala mbalimbali yanayohitaji usaidizi wa kisheria.
Akiainisha masuala makubwa yanayowakabili wanancho wa ubungo ni pamoja na migogoro ya ndoa, ardhi, Mirathi, pamoja na migogoro ya kibiashara, hivyo uwepo wa programu hii kwa wananchi ni msaada mkubwa kwa Serikali kutatua changamoto hizo ambazo kimsingi zilipaswa zishughulikiwe na serikali.
Kutokana na umuhimu huo, Mhe. Kheri amewasisitiza wenyeviti, watendaji wa kata na mitaa kutoa ushirikiano kwa wanasheria hao ikiwemo kuwatangazia wananchi kuhusu uwepo wa huduma hiyo ili waweze kutumia fursa hiyo adhimu bure kabisa.
Aidha, akitoa maelezo ya ushiriki wao, Mkurugenzi wa kampuni ya NMG Artoney ndugu Gerald Noah amesema wao wapo tayari kutoa msaada huo wa kisheria kwa wananchi wa Ubungo na amemshukuru Mkuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano walionesha kwa kuwapokea na kuwaruhusu kutoa huduma ya kisheria kwa wanaubungo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya ubungo ndugu Beatrice Dominic amewapongeza wanafunzi na mawakili hao kwa moyo wao wa kizalendo wa kutaka kuwahudumia wananchi kwenye eneo nyeti la usaidizi wa kisheria
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa