#Repost @ortamisemi with @let.repost
• • • • • •
Na. Fred Kibano - OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 jan Ijumaa tarehe 14 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.
Akiwasilisha Bajeti hiyo, Waziri Kairuki ameomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 9,144,021,699,000 (Trilioni Tisa) ambazo ni matumizi ya kawaida ya Ofisi, mishahara ya watumishi, Mikoa, Halmashauri, Tume ya Utumishi wa Walimu na Miradi ya Maendeleo.
Waziri Kairuki ametoa maelezo ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2022/2023 kuwa katika eneo la Usimamizi na Uendeshaji wa Elimumsingi wanafunzi wa Elimu ya Awali waliandikishwa 1,411,810, sawa na asilimia 103.52 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,363,834 ukilinganisha na mwaka 2023 ambapo wanafunzi 1,500,227 wameandikishwa ikiwa ni asilimia 109.37 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,371,690 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,411 ikiwa 1,211 wasichana na wavulana 1,200.
Waziri Kairuki amesema mafanikio ya kuandikisha wanafunzi wengi kwa ongezeko la wanafunzi 88,417 sawa na asilimia 3.38 ikilinganishwa na wanafunzi walioandikishwa mwaka wa 2022 yametokana uhamasishaji wa Jamii, ujenzi wa vituo shikizi na kuendelea kutoa ElimuMsingi Bila Ada.
Kuhusu afya ya Msingi, Waziri Kairuki amesema katika mwaka 2022/23 ziliidhinishwa Shilingi Bilioni 143.15 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Afya ya Msingi ambapo hadi Februari, 2023 Shilingi Bilioni 124.10 zimepokelewa sawa na asilimia 86.69 ya fedha iliyoidhinishwa.
Waziri Kairuki amesema Shilingi Bilioni 69.95 ziliidhinishwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 15.15 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa zahanati 300, Shilingi Bilioni 47.70 kwa Vituo vya Afya 159 na Shilingi Bilioni 7.10 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vya afya ya kinywa, meno na macho kwa hospitali za Halmashauri 71 zilizokamilika na hadi kufikia Februari, 2023.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa