TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE AMBAO LESENI ZAO ZIMEISHA MUDA WA KUTUMIKA WANATAKIWA KUHUISHA (RENEW) LESENI NA WASIO NA LESENI KUWA WANAPASWA KULIPIA LESENI ZAO ZA BIASHARA KABLA YA TAREHE 21/07/2019. VILE VILE WANATAKIWA KULIPIA USHURU WA HUDUMA YAANI “SERVICE LEVY”. MALIPO YAFANYIKE KATIKA OFISI ZA BIASHARA ZILIZOPO MAKAO MAKUU KIBAMBA AU KATIKA OFISI NDOGO ZA BIASHARA ZILIZOPO STENDI YA MABASI MAWASILIANO, SIMU 2000.
AIDHA KILA MFANYABIASHARA ANATAKIWA KUWA NA LESENI YA BIASHARA KWENYE BIASHARA YAKE KWA KUWA HALMASHAURI ITAFANYA UKAGUZI WA BIASHARA ZOTE KUANZIA TAREHE 22/07/2019 IKIWA NI UTEKELEZAJI WA SHERIA YA BIASHARA NA. 25 YA MWAKA 1972.
YOYOTE AMBAYE ATABAINIKA HAJAHUISHA LESENI YAKE AU ANAFANYA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE IKIWA NI PAMOJA NA KULIPA PENATI NA FAINI ISIYOPUNGUA 200,000/=
LIPA LESENI YA BIASHARA YAKO KUEPUKA USUMBUFU
IMETOLEWA NA:
UTAWALA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa