• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mipango miji na Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Utumishi na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Maji na Usafishaji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
        • Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Vipeperushi
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WAMILIKI VITUO VYA KULELEA WATOTO (DAYCARE) WAPEWA MAFUNZO

Posted on: January 23rd, 2021

Wamiliki wa vituo vya watoto walio chini ya miaka mitano (DAYCARE) katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam, wamepatiwa mafunzo maalumu  yanayolenga kufahamu sheria, kanuni na taratibu na miongozo ya uendeshaji wa vituo hivyo ili kutoa huduma bora  ya malezi kwa watoto.

Mafunzo hayo yametolewa leo januari 23, 2021 na Manispaa ya Ubungo kupitia idara ya afya na ustawi wa jamii ambapo wamiliki 321 kati ya 600 wameshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi  wa Lapaz mtaa  wa Luguluni.

Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto  wadogo mchana maarufu kama Daycare wapatiwa mafunzo juu ya taratibu kanuni na sheria za kuendesha vituo hivyo.


Akitoa maelezo wakati wa kufungua mafunzo hayo Afisa ustawi  wa Manispaa ya Ubungo Zainabu Masilamba , alisema kuwa Manispaa kupitia kitengo cha ustawi wa jamii imeamua kuendesha mafunzo kwa wamiliki hao kutokana na ongezeko kubwa la uanzishwaji wa  vituo hivyo  vya kulelea watoto wadogo ambavyo havina usajili  jambo ambalo ni kinyume na taratibu.


Masilamba alieleza kuwa, kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2014 sura ya 13 kupitia sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 inaelekeza ili  kituo cha kulelea watoto wadogo mchana kiweze kufanya kazi lazima kuzingatia vigezo ambavyo vitamwezesha mtoto kuwa katika mazingira salama ya kujifunza elimu ya malezi ya  awali


Baada ya mafunzo haya ya kujenga uelewa, tunategemea wamiliki wa vituo ambavyo vinaendeshwa kinyume na taratibu, sheria na miongozo watatumia muda huu uliobaki kurekebisha kasoro zilizopo ili wasifungiwe vituo wakati wa zoezi la kufunga vituo visivyo na sifa mwishoni mwa mwezi machi.

Masilamba  anasema " tarehe 24 machi mwaka huu,  Manispaa ya Ubungo itafunga vituo vyote ambavyo vinaendesha huduma ya kulea watoto wadogo mchana kinyume na taratibu, kanuni miongozo na sheria ya kuendesha vituo hivyo ikwemo kutosajiliwa na kuto kidhi vigezo vya kutoa huduma ya  malezi ya awali kwa  watoto wadogo"

Aidha wamiliki wamekumbushwa kuzingatia ukubwa wa  eneo litakalo mwezesha mtoto  kujifunza kwa vitendo, uwepo wa miundombinu mizuri  hasa vyoo, usafi wa mazingira na pamoja na kuwa na  walezi waliopata mafunzo katika vyuo vya Montesol vinavyotambulika na serikali na kamishina wa ustawi wa jamii.

Wito umetolewa kwa wamiliki wa vituo vya kutoa huduma ya malezi ya awali kwa watoto wadogo mchana kutochanganya (daycare) na huduma zitolewazo katika shule za awali (nursery school) ikiwemo kuandika

Frank Andrea Kimaro ni kati ya wamiliki wa vituo waliopata mafunzo hayo, ameeleza kuwa mafunzo  hayo yamemuongezea uelewa zaidi wa namna ya kuendesha kituo chake lakini pia vitu au huduma anayostahili mtoto mdogo kutoka kwenye kituo.

Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo 606  vinavyotoa huduma ya kulea watoto  wadogo mchana na kati hivyo ni vituo 100 vimesajiliwa 


Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Peter Nsanya akisisitiza jambo kwa wamiliki wa vituo wakati wa mafunzo. Amewakumbusha umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) ili kuwa na uhakika wa matibabu kwa gharama nafuu. 

Taarifa

  • HUDUMA YA KUKODI GARI LA MAJI TAKA June 12, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA August 12, 2019
  • Tangazo la ukataji au kuhuisha leseni na Tozo mbalimbali. December 08, 2017
  • Uchangiaji Damu Hospitali ya Sinza June 14, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KITUO KIPYA CHA MABASI MBEZI LUIS KUANZA KUTOA HUDUMA TAREHE 25 FEBRUARI, 2021

    February 21, 2021
  • WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA KWA UFANISI KUZALISHA WASOMI BORA

    February 16, 2021
  • BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA UBUNGO LAZINDULIWA RASMI

    February 15, 2021
  • ENG NYAMHANGA APONGEZA UJENZI WA MADARASA 9 KING'ONGO, AAHIDI FEDHA ZA UJENZI WA MADARASA MENGINE 6-8

    February 12, 2021
  • Tazama zote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kibamba Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa