USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (HOTEL LEVY)
· Ushuru huu unalipwa kwa kufuata Sheria ya nyumba za kulala Wageni(The Hotels Act) ya mwaka 1965 sura ya 105 kifungu cha 26 (2) pamoja na Marekebisho yake ya mwaka 2002 (The Hotel Act Wap. 105) toleo la mwaka2002.
· Asilimia 20% ya jumla ya Mapato yanayotokana na malipo ya watejawanaolala kwenye nyumba husika ya wageni hutozwa ushuru kwa kila mwezi.
· Mlipaji wa ushuru huo ni mmiliki wa Biashara ya nyumba hiyo ya kulalawageni. Malipo hayo kufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 ya kila mwezi.
Taratibu za Ushuru wa Nyumba za kulala wageni ni kama ifuatavyo:-
· Mfanyabiashara wa nyumba ya kulala Wageni anapaswa kujaza Kitabu chaWageni wanaolala au kuingia kwenye nyumba hiyo kila siku (visitors book).
· Mwendesha Biashara ya nyumba ya kulala wageni anatakiwa ajaze fomu zawageni wanaopangisha hapo kila siku (Daily occupancy Return) na za kila mwezi(Monthly occumpancy Return).
· Ushuru huu hulipwa na Wafanyabiashara wa Nyumba za kulala wageniambao hawajasajiliwa kulipa VAT.
Adhabu:
· Asilimia 25% ya Ushuru wa Hoteli. Itatozwa endapo mlipajiatakuwa amechelewa kulipia zaidi ya siku saba kifungu cha 32(a).
· Ongezeko la asilimia 10% itakayokuwa inaongezeka kwa kiwango cha Adaambayo haijalipiwa kwa kila siku thelathini (kifungu cha 32 (b) kinaelekeza.
· Kukiuka taratibu za ulipaji wa Hoel levy faini ni Sh. 500,000/= (lakitano). Mfano kudanganya mapato, kutokuwa na kitabu cha kumbukumbu nk.
· Kukiuka ulipaji wa Hotel Levy faini ni Shs. 2,000,000/= Mfano; Nyumbaya Wageni ambao haijalipa Hotel Levy tangu kuanzishwa kwake.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa