KITENGO CHA UCHAGUZI KATIKA SERIKALI ZA MITAA (HALMASHAURI ZA WILAYA, MIJI, MANISPAA NA MAJIJI)
Kitengo cha Uchaguzi katika Serikali za Mitaa ngazi ya Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji kinaratibu shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu pamoja na Chaguzi zote ndogo zote. Yapo majukumu mengi ya kila siku na yale yanayojitokeza nyakati za Uchaguzi na kabla ya Uchaguzi kama ifuatavyo:-
1. Kuanisha nafasi wazi za viongozi wa Vijiji, Mitaa, Vitongoji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi na TAMISEMI,na kuzifanyia mchakato wa uchaguzi mdogo.
2. Kuratibu chaguzi ndogo za serikali za Mitaa (Vitongoji, Vijiji na Mitaa) pamoja na chaguzi ndogo katika Majimbo ya Uchaguzi (Madiwani na Wabunge).
3. Kutoa Matangazo ya nafasi wazi kwa vyama vyote vya siasa vyenye Usajili wa Kudumu.
4. Kutoa mafunzo ya Utawala bora kwa viongozi wote wa kuchaguliwa mara kwa mara.
5. Kusimamia Utendaji wa Serikali za Mitaa ngazi ya vitongoji vijiji, Mitaa na Kata.
6. Kutoa taarifa na Ushauri wa mwenendo wa Serikali za mitaa kwa Mamlaka.
7 Kuandaa Ratiba ya Uchaguzi na kusambaza kwa vyama vya Siasa na wadau wengine vikiwemo vyombo vya Usalama.
8. Kuratibu Uteuzi wa Wagombea katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
9. Kuratibu Uanzishwaji wa Maeneo Mapya ya Kiutawala ikiwa ni pamoja na kuanisha Maeneo ya Utawala ya Mipaka ya Kiutawala ya Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji kwa ajili ya Maandalizi ya VITUO vya kuandikishia na kupiga kura.
10. Kuratibu Mkutano wa kwanza wa chaguzi za Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya mara baada Uchaguzi.
11.Uhakiki endelevu wa vitambulisho vya wapiga kura (waliofariki), Kwa waliopoteza na wanahitaji vitambulisho vingine wananchi wanaelekezwa kwenda Tume ya Taifa baada ya kujiridhisha kuwa wanastahili Kupatiwa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa