Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba akiwa ameambatana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama pamoja na timu ya wataalamu ya Manispaa ya Ubungo ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, wamekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika Manispaa ya Ubungo.
Ziara hiyo imefanyika mapema leo Machi 31, 2023 ambapo miradi 11 ya maendeleo imbayo inatekelezwa kwenye Manispaa ya Ubungo kwenye sekta mbalimbali za Maendeleo imekaguliwa na timu hiyo
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na miradi ya sekta ya Afya, sekta ya miundombinu ya usafiri, sekta ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, sekta ya maji pamoja na sekta ya Mazingira
Akikagua mradi wa tenki la maji la mshikamano, mradi uliogharimu Bilioni 4.5. Mhe. Komba ameipongeza DAWASA kwa kazi kubwa waliyofanya kwenye ujenzi wa mradi huo na pia amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Bilioni 2.5 kutoka kwenye fedha za mradi wa uviko19 ili kuwezesha kujengwa kwa mradi huo muhimu kwa ustawi wa maisha ya wanaubungo.
"Mhe. Rais ametuletea fedha hizi za ujenzi wa mradi huu mkubwa wa maji, ni jukumu letu kuulinda mradi huu ili tija yake ionekane kwa wananchi. Na ninawaagiza DAWASA kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuwaunganishia maji wananchi ambao hawajafikiwa bado" alisema Komba
Aidha wajumbe walioambatana katika ziara hiyo wamefurahishwa na viwango vya miradi iliyoakaguliwa na pia wametoa ushauri wa kushughulikia changamoto chache zilizoonekana.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa