Maafisa ugani waliopo kwenye kata zote 14 na mitaa yote 90 ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wamekumbushwa juu ya umuhimu wa kuwa waadilifu, uwajibikaji na kuongeza ubunifu kwenye kazi za kila siku za kutoa huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi wa Manispaa ya Ubungo
Hayo yamesemwa leo Februari 20, 2023 na mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba alipokutana na maafisa ugani hao na kuongea nao
Aidha Mhe Komba ameweka utaratibu kwa maafisa hao kuanza kutoa ripoti za kila wiki kwa shughuli zao wanazozifanya kwenye vituo vya kazi, na utaratibu huo unaanza mara moja
Vilevile Mhe Komba amewaagiza maafisa elimu kata kuanza kufanya maandalizi ya kufanya makongamano na wadau wa elimu ili kufanya tathmini ya kiwango cha ufaulu wa shule zote za msingi na sekondari pamoja na kuweka mikakati ya kuongeza ufaulu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa